HADITHI: SIDE MCHORAJI 6
Madam Claudia hakuelewa kabisa namna picha ile ilivyopotea, alijaribu kuwashirikisha wenzake kuhusu mkasa ule lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kumpa jibu au wazo zuri la kumsaidia kuipata picha. Wengine walihisi atakuw ameipoteza mwenyew, huku wengne wakihis imeibiwa. Alitoa taarifa kwenye uongoz wa hotel kuhusu kupotea kwa picha ili kama itapatikana aweze kurudishiwa.
siku iliyofuata....
Madam Claudia pamoj na wenzke walikuw na safari ya kuelekea kwenye mapango ya asili ya Amboni yaliyokuwepo umbali wa kilomita 7 kutoka pale hotelini walipofikia.
Safari ilianza, na kabla hawajafik mbali Madam anakumbuk jambo, anaitoa simu yke haraka kutok kwenye handbag na kufungua faili la picha (gallerly). Anakutana na picha ya mchoro ule uliopotea kimaajabu ambao aliupiga picha usiku wa jana. Wazo la kurudi kwa kijana Side ili amchoree tena linamjia kichwani, Hakutaka kukawia kabisaaa Safari ilikuw bado mbichi, Hvyo aliwaomba wenzie ili wapitie kwa kijana Side ili aweze kumkabidhi picha ile. Haikuw rahis wenzke kukubali kutokana na ubovu wa barabara ya kuelekea kibandani kwa side na ukizingatia ilikuw ni msimu wa mvua,baada ya mvutano kidogo ndipo walimkubalia kwa shingo upande kwa sharti moja tu, Gari halitoingia mpaka kibandani kwa Side badala yake litasimama mbali kidogo ilipoishia barabara ya changarawe. Madam alikubali na walipofika mwisho wa chanagarawe aliteremka pamoja na mkalimani mmoja na kutembea takriban mita 700 mpk kufikia kibandani kwa Side.
Kwa bahati mbaya Walimkuta Osama peke yake...........
Side alikuw ametoka kdg kwenda kununua chakula. Osama aliwakaribisha na baada ya dakika chache Side alirejea. Kutokana na kuw na muda mchache sana! Madam hakuweza kumweleza chochote kuhusu kupotea kwa picha ile ya awali. Alichomwambia ni kwamba anahitaji kuchorewa picha kama ile ya mwanzo, Alimuuliza kama ana simu inayosupport Bluetooth ili aweze kumtumia picha. lakini Side hakuwa na simu kabisaaa, simu yake ilikufa miezi miwili iliyopita, kipindi chote hiko alitumia simu ya rafiki yake Osama ambayo nayo pia haikuwa na Bluetooth, Mkalimani hakujua moyo wa uaminifu kwa kijana Side Madam aliutoa wapi, kwani alimkabidhi simu yke (iphone) iliyokuw na picha ile ili kaz yake ifanyike vizuri. kisha Madam alitaka kufaham ni muda gani itakuw tayar, Side hakupenda kuw muongo alimwelez madam kuhusu kutokuwepo kwa baadhi ya rangi na vifaa ambavyo sehemu pekee ya kuvipata ilikuw ni mjini. hivyo angechelewa kdg kumaliza, Aliomba apewe siku 3 na pesa kidogo ya kununua vfaa hvyo. Madam alimkabidhi Side kiasi cha sh.lak 1, kwa ajili ya kununua rangi na vifaa na kumuahidi kumlipa nyingne siku atakayofuata picha ile.

Baada ya kumalizana na Side anarudi chap kwa wenzke kisha safari inaendelea.
*******************
Baada ya madam kuondoka, Side hakulaza damu, Alimalizia kazi ndogo ndogo za pale kibandani huku nyingine akimuomba Osama azikamilishe kisha anamuaga mwenzke na kurudi ghetto ili kujiandaa na safari ya mjini.
Alipofika Ghetto...
Anabadili nguo chap! na kuingia bafuni kujimwagia, ndani ya dakika tatu alikuwa ashamaliza zoezi hilo na tayari alikuwa ndani akijipaka mafuta yake ya mgando aina ya baby care huku akichakura begi lake chakavu kutafuta nguo ya kuendea mjini. Nguo zake nyingi zilikuwa na madoa ya rangi kutokana na kuchafuka kazini, Aliipata suruali moja iliyokuwa yenye unafuu kidogo, anaisogeza karibu na pua na kugundua ina nukia harufu ya ufundo kutokana na kutovaliwa kwa kipindi kirefu, anaivaa hivyo hivyo na kumalizia na shati lililojikunja kama lilitoka mdomoni mwa ng'ombe, hakuwa na pasi ya umeme wala ya mkaa, alichofanya ni kuikung'uta na kuivaa. Anachukua chanuo na kipande cha kioo kilichokwisha vunjika ili kuziweka sawa nywele zake. wakati anaendelea kuziweka sawa nywele zake alihisi kitu kikimtekenya tekenya sehemu za siri, anavua kwa spidi ile suruali huku akirusha miguu huku na huko mara ghafla anamuona mende mkubwa akitoka kwenye suruali na kukimbilia chini alipokuwa ameegesha godoro lake. Anamuua yule mende na kumtupa nje lakini alipokuja kuitazama ile suruali katikati ya miguu ilishararuka kidogo kutokana na kuvuliwa pasipo ustaarabu. Hakuwa na nyingine aliipigilia mwilini na kutoka nje. Anauegesha mlango wake taratibu kutokana na bawaba moja ya chini kukatika, kisha anamalizia kwa kuufunga na kufuli yake ya solex na safari ya kuelekea stendi ikaanza.
Anafika mpaka stendi na kuanza kungojea gari ya mjini, zinapita dakika 15 pasipo kuona gari yeyote, anajaribu kubadilishana mawazo na wafanya biashara ndogo ndogo wa eneo lile ambao wanamkatisha tamaa zaidi kwa kumwambia amechelewa kidogo, muda aliofika ndipo gari ile ya mjini ilikuwa imetoka pale, amechelewa itabid asubiri gari ya mwisho inayoweza kuja ama isije kutokana na hali ya hewa ya mvua. Side aliyekuwa na hamu kubwa ya kuanza kazi ya Madam mapema, ilibidi akomae pale kuisubiri hyo gari ya mwisho. Ananyanyua mkono wake wa kushoto na kuupeleka karibu na uso na kwakutumia vidole viwili vya mkono wa kulia anabofya kitufe cha saa yake ya kimulimuli ili kujua muda, Oh my God! Ilishatimia saa 8.34 mchana.........
Sasa ni saa 9.15, yamekatika masaa mawili na dk 48 tangu alipofika stendi, Akawa anatafakari kuahirisha safari, ghafla inapaki taxi karibu kidogo na aliposimama Side kisha kioo kinafunguliwa, Mzee mmoja wa makamo anatoa sura nje na kumuita kwa ishara ya mkono. Side anasogea mpaka karibu kabisa na gari lile ili kumsikiliza mzee yule,
Mzee: Hujambo kijana...(Huku akimwangalia kupitia juu ya miwani aliyokuwa ameivaa)
Side: Sijambo,Shikamoo mzee
Mzee: Marahaba, samahani kijana!... (akavuta pumzi kidogo)
Mzee: Unapafahamu Kilaweni?
swali hilo lilikuwa rahisi sana na kwa Side aliyemaliza vijiji vyote vya mkoa ule kutokana na kazi zake za uchoraji pamoja na saidia fundi pale ambapo alikosa dili za uchoraji. Alimjibu kuwa anakifahamu vizuri na walipomweleza smtaa waliokuwa wanaelekea pia nao aliufahamu na kuwaelekeza, mzee yule alimshukuru sana Side kwa msaada wake na wakati anaondoka alimuuliza mahali anapoelekea ili amsogeze, Side alimwambia kuwa anaelekea mjini na ilikuwa ni kama bahati kwa Side kwani kijiji cha Kilaweni hakikuwa mbali sana na mjini, Hvyo mzee yule alimpa lift. Wakati wakiwa njiani walipiga stori nyingi mzee yule alikuwa mchangamfu sana,, mzee alitaka kufahamu Side anajishughulisha na nini, Side alimtajia kazi yake bila kuficha na mzee alifurahi sana kukutana na kijana mwenye kipaji ambacho yeye alinyimwa, na kwa utani akamuahidi atamtafuta siku moja ili amchore picha yake kama alivyo, mwisho walibadilishana namba ambapo Side alimpa namba ya rafiki yake Osama na kudai kuwa simu aliisahau ofisini kwake. Mzee alinogewa na stori za Side na ilipofika sehemu ya kuachana hakuona sababu ya kumshusha Side kwani angepata shida ya usafiri mpaka kufika mjini, alimpeleka mpaka mjini kisha yeye akarudi ili kuelekea Kilaweni iliyokuwa nyuma ya mjini.
********************
Inasimama Hiace moja chakavu kituoni na kijana mmoja aliyekuwa na mizigo mingi anateremka pamoja na abiria wawili watatu kisha gari ile inaendelea na safari. Saa ya mkononi ilisema Saa 12.46, vijana wabebaji wa mizigo pale stendi wanamkimbilia ili kujaribu riziki zao, hata hvyo kijana yule anagoma kubebewa na kuanza kujitwisha mizigo peke yake. Alionekana amechoka sana na ndipo kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Suma Alimpokea ile mizigo bila kuombwa na kumuambia maneno haya kijana yule
"Side acha nikusaidie rafiki yangu unaonekana umechoka sana, usinipe chochote, siku nikija kutaka huduma kwako utanifanyia punguzo"
Side alicheka sana lakini hakuwa na jinsi, Suma ndo alishaichukua mizigo yote ya kichwani na kumuachia michache sana ya mkononi. na safari ya kuelekea kibandani ikaanza. Walifika pale kibandani na kukutana na Timbwili zito, Osama pamoja na Mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la mzee Mushi walikuwa kwenye mzozo mkubwa huku watu kibao wakizunguka kibanda cha side kushuhudia ugomvi ule.......Osama alikuwa amechafuka tope mwili mzima
Je nini Kimetokea...USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA....
mtunzi: John J Kiwovele

Reviewed by PLATO ACADEMY
on
02:12
Rating:
No comments: